LYRIC

Ooh mwanamke nyumba ndogo
Umenifika kwa koo!
We mwanamke mwenzangu (Uuh Uh!)

Nasema Ooh! Ooh! mwanamke nyumba ndogo
Umenifika kwa koo!
We mwanamke mwenzangu (Uuh Uh!)

Hawezi kulalamika, kila akija nyumbani
Mkewe mimi hupika, kuja kwako ni utani
Kwangu kanipendea akili, mrembo tena laini
Huyu ni wangu dada pole, usiniletee kisirani

Samahani, samahani mwanzoni
Sitaki wewe ujitambulishe wataka nini?
Mie ndo mke wa kwake nyumba kubwa
Tena nimemkwama mwenzangu kama kamba nimefungwa

Una ubaya, una ubaya nami
Unaniudhi wanikera bure
Una ubaya, una ubaya nami
Unaniudhi wanikera bure

Using’ang’ane na mimi
Ni haki yangu jamani nikujulishe mi chui
Mie nikiwa ndo bibi kwangu haiwezekani
Kwangu bwana anabaki

Sitaki usaidizi wala usinichokoze
Siwezi kumshare mume ndo hivyo mwanamke
Jihadhari chunga sana mwezangu
Usinipate

Una ubaya, una ubaya nami
Unaniudhi wanikera bure
Una ubaya, una ubaya nami
Unaniudhi wanikera bure

Che, che che
Unapenda vitu vya che
Unapenda doze doze
We mwanamke unanikera

Nasema che, che che
Unapenda vitu vya che
Unapenda doze doze
We mwanamke unanikera

Wewe mtoto wa kike
Wacha kumshare share
Wewe mtoto wa kike
Wacha kumshare share

Nasema twende tingisha, we tingisha
Mama mboga tingisha, wewe mama tingisha
Sasa Amira tingisha, we tingisha
Na twende Fari tingisha, we tingisha wewe

Added by

yanson

SHARE

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *

PUBLICITE