LYRIC

Moyo umekua sugu hadi maumivu yanadunda
Siogopi waongo sipokei
Wakweli mapenzi yamenifunza
Tamu imekua chungu moyo ulifanywa punda
Hadi mizigo ya kokoto
Ikanichosha mwili machozi nikafuta

Sio kama siogopi kuumia tatizo nishaumia sana
Mapenzi ya maharamia nikachukia ujana
Kuna muda nawaza rudia tatizo nikipenda sana
Ndo nafasi wanaitumia kuniumiza mchana

Na usiku usingizi sipati, nakesha
Usiku nalia bahati sina (Nakesha)
Bora pombe mapenzi sitaki (Nakesha)
Ya nini kuumia bora nile dawa (Nakesha)

Kila napotarajia nitafurahia
Ndo nazisisha
Maumivu kwa ndani mwili umekufa ganzi
Kila pendo naloingia
Yanajirudia kunikatisha
Nikatisha tamaa mnyonge mwana simanzi

Kama ningeliweza kuchagua
Utotoni ningeamua
Bora hata nisingeyajua
Yataniua mapenzi

Sio kama siogopi kuumia tatizo nishaumia sana
Mapenzi ya maharamia nikachukia ujana
Kuna muda nawaza rudia tatizo nikipenda sana
Ndo nafasi wanaitumia kuniumiza mchana

Na usiku usingizi sipati (Nakesha)
Usiku nalia ah, bahati sina (Nakesha)
Bora pombe mapenzi sitaki (Nakesha)
Ya nini kuumia bora nile dawa (Nakesha)

Mapenzi sitaki (Nakesha)
nakesha…

Added by

yanson

SHARE

Comments are off this post